Moravia

ardhi ya kihistoria katika Jamhuri ya Czech
Pitio kulingana na tarehe 23:49, 24 Novemba 2009 na MelancholieBot (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: fa:موراویا)

Moravia (Kicheki na Kislovakia: Morava; Kijerumani: Mähren; Kihungaria: Morvaország; Kipoland:Morawy) ni mkoa wa kihistoria katika mashariki ya Ucheki. Jina limetokana na mto Morava.

Bendera ya Moravia
Moravia katika jamhuri ya Uceki

Pamoja na Bohemia eneo la Moravia ni sehemu muhimu ya Ucheki ambayo ni nchi iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya Slovakia kutoka katika Chekoslovakia.

Mji mkuu wa Moravia ni mji wa Brno (Kijer.: Brünn).

Moravia ilikaliwa na makabila ya Waslavoni tangu karne ya 6. Katika karne ya tisa dola la Moravia lilikuwa himaya muhimu zaidi kati ya Waslavoni wa Ulaya. Mwanzo wa karne ya 10 himaya iliporomoka kati ya uenezaji wa Wajerumani upande wa magharibi na Wahungaria upande wa mashariki-kusini.

Katika kare zilizofuata Moravia ilikuwa chini ya athira ya Poland au Ujerumani ikaishia kuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma na tangu 1526 chini ya utawala wa familia ya Habsburg.

Tangu 1918 Moravia ilikuwa jimbo la nchi ya Chekoslovakia, tangu 1993 ya Ucheki.

Kigezo:Link FA