Aleksanda wa Yerusalemu

Aleksanda wa Yerusalemu (Kapadokia, leo nchini Uturuki, karne ya 2Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli 251 hivi) alikuwa askofu wa Yerusalemu kwa miaka mingi hadi kifodini chake[1]. Mjini Yerusalemu alianzisha maktaba muhimu na chuo.

Picha takatifu ya Mt. Aleksanda wa Yerusalemu.

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu mfiadini na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Machi[2] au 22 Desemba[3][4].

Maisha

hariri

Aleksanda alizaliwa katika familia ya Kipagani akapata elimu bora iliyomfanya ajue falsafa na dini mbalimbali hadi akajiunga na Ukristo.

Hapo alikwenda Misri kuhudhuria Chuo cha Kikristo cha Aleksandria akafahamiana na Origen. Huko alifungwa hadi mwaka 211 kutokana na dhuluma ya kaisari Septimius Severus.

Mwaka 212 alifika Yerusalemu akawa askofu mwandamizi wa Narsisi wa Yerusalemu[5][6], na baada ya kushika uongozi kamili wa jimbo alishughulikia elimu ya Kikristo kwa kuanzisha shule na maktaba kwa mfano wa Aleksandria[7]. Pia alimtetea Origen na kumpa upadirisho.

Dhuluma mpya za kaisari Decius zilipoanza alifungwa tena na kuteswa hadi kuuawa bila kujali uzee wake[8] hata akafariki kifungoni[9].

Maandishi yake

hariri

Kati ya maandishi yake mengi, zimetufikia sehemu tu za barua nne katika vitabu vya Eusebi wa Kaisarea[10][11][12].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/45870
  2. Martyrologium Romanum
  3. (Kigiriki) Ὁ Ἅγιος Ἀλέξανδρος ὁ Ἱερομάρτυρας Ἀρχιεπίσκοπος Ἱεροσολύμων. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
  4. (Kigiriki) Ὁ Ἅγιος Ἀλέξανδρος ὁ Μάρτυρας. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
  5. Eusebi wa Kaisarea, Historia Ecclesiastica, VI, 11; Sokrate Mwanashule, Historia Ecclesiastica, VII, 36
  6. Monks of Ramsgate. “Alexander of Jerusalem”. Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 24 May 2012
  7. Eusebi wa Kaisarea, Historia Ecclesiastica, V, 20
  8. Campbell, Thomas. "St. Alexander." The Catholic Encyclopedia Vol. 1. New York: Robert Appleton Company, 1907. 22 Sept. 2012
  9. Christie, Albany James (1867). "Alexander". In William Smith. Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology. 1. Boston: Little, Brown and Company. pp. 115. Archived from the original on 2007-05-18. https://web.archive.org/web/20070518080152/http://www.ancientlibrary.com/smith-bio/0124.html. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-18. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  10. Eusebius, Ecclesiastical History, vi. 11.
  11. Eusebius, "Ecclesiastical History, vi. 14"
  12. Eusebius, "Ecclesiastical History, vi. 19"

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.