Alfonso Rodriguez
Alfonso Rodríguez, S.J. (Segovia, 25 Julai 1532 – Palma de Majorca, 31 Oktoba 1617) alikuwa Mkristo wa Hispania aliyejiunga na Wajesuiti kama bradha,
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1825, na mtakatifu tarehe 15 Januari 1888.
Maisha
haririRodríguez alikuwa mtoto wa mfanyabiashara ya sufu. Mtakatifu Petro Faber, mmoja wa waanzilishi wa Shirika la Yesu, alipofika kuhubiri Segovia, familia ya Rodriguez ilimkaribisha. Faber alimuandaa kijana Alfonso kwa Komunyo ya Kwanza.[2]
Alipokuwa na umri wa miaka 14, baba alifariki, hivyo Alfonso aliacha shule amsaidie mama katika biashara.[3]
Alipofikia miaka 26 alimuoa María Suarez, aliyemzalia watoto watatu.
Alipofikia umri wa miaka 31 alibaki mjane mwenye mtoto mmoja tu bado hai.
Tangu hapo alishika maisha ya sala na toba, akijitenga na ulimwengu.
Alipofiwa mtoto aliyebaki, alianza kusikia wito wa utawa.[4]
Kwa ajili hiyo, akiwa na miaka 39 alijaribu kurudi masomoni, lakini hakufaulu, pia kwa sababu ya ugumu wa malipizi yake ulioharibu afya yake.
Hatimaye, tarehe 31 Januari 1571, akiwa na miaka 40, alipokewa na Wajesuiti.[4] Hoja ya mkuu aliyemkubali kinyume cha taratibu ilikuwa kwamba, kama Alfonso hafai kuwa bradha au padri, anaweza kuingia awe mtakatifu.[2]
Aliweka nadhiri za daima mwaka 1585 akiwa na miaka 54.
Kwa miaka 46 alifanya kwa namna bora kazi ya bawabu katika shule ya bweni ya Palma de Majorca, katika visiwa vya Baleari, akiwajenga wanafunzi na watu wote waliofika huko kwa unyenyekevu, utiifu, sadaka ya kudumu na kwa mashauri yake mazuri ajabu. Mmojawao ni Petro Claver, aliyeelekezwa naye kwenda Amerika kama mmisionari[5].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 2.0 2.1 Martin SJ, James. "The Catholic Brothers and St. Alphonsus Rodriguez", America, October 28, 2010
- ↑ "Ghezzi, Bert. Voices of the Saints, Loyola Press, ISBN 978-0-8294-2806-3". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-29. Iliwekwa mnamo 2016-09-24.
- ↑ 4.0 4.1 Campbell, Thomas. "St. Alphonsus Rodriguez." The Catholic Encyclopedia. Vol. 1. New York: Robert Appleton Company, 1907. 2 Apr. 2013
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/75650
Marejeo
hariri- Holweck, F. G., A Biographical Dictionary of the Saints. St. Louis, MO: B. Herder Book Co., 1924.
Viungo vya nje
hariri- Jesuit Brothers Archived 2013-06-20 at Archive.today
- "St. Alphonsus Rodriguez", Living Space, Irish Jesuits
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |