Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (ing. United Nations General Assembly) unaunganisha wawakilishi wa nchi zote ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Ukumbi wa Mkutano Mkuu wa UM
Mkutano Mkuu ulihubiriwa na mjumbe wa taifa mwanachama

Tarehe ya Mkutano Mkuu

hariri

Mkutano huu hufanyika mara moja kwa mwaka kwa kawaida kuanzia Septemba hadi Desemba kwenye makao makuu ya UM mjini New York, Marekani. Mkutano Mkuu wa kwanza ulifanywa tarehe 10 Januari 1946.

Kazi ya Mkutano Mkuu

hariri

Mkutano Mkuu una wajibu wa kuchungulia na kuamulia makisio ya mwaka wa UM, pia kuamulia maazimio yenye hadhi ya mapendekezo. Mkutano Mkuu unaweza kujadili mambo yote ya kimataifa ambayo hayajadiliwi na Baraza la Usalama la UM.

Maazimio ya Mkutano Mkuu hayana uzito kama haki au sheria ya kimataifa, tofauti na maazimio ya baraza la Usalama. Lakini yanaweza kupata umuhimu mkubwa kama mataifa mengi sana yanayaunga mikono. Maazimiio yanayohusu mambo ya ndani ya utawala wa UM yanapasakutekelezwa na Katibu Mkuu wa UM na idara zake.

Maazimio na kupiga kura

hariri

Kila nchi mwanachama inaweza kuingia na wawakilishi 5 lakini wakati wa kupiga kura kila nchi ina kura moja. Hakuna tofauti kama nchi ina wakazi wengi (kama China yenye wakazi zaidi ya bilioni 1) au wachache (kama Tuvalu yenye wakazi 10,600). Katika maswali yaliyo muhimu azimio linahitaji theluthi mbili za kura za mkutano.

Utaratibu huu unahusu maswali kama vile

  • Mapendekezo kuhusu amani duniani na usalama wa kimataifa
  • Uchaguzi wa nchi wanaoingia kwa muda katika Baraza la Usalama na mabaraza mengine ya UM
  • kukubali nchi kuwa mwanachama wa UM
  • kusimamisha haki za uanachama wa UM kwa nchi inayopuuza masharti yaliyoelezwa katika katiba ya UM au hata kutenga nchi kabisa
  • maswali yote ya makisioya UM

Katika maswali mengine azimio linapokelewa kwa kura nyingi za kawaida.

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: