Nenda kwa yaliyomo

Kiawentiio : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Anzisha Makala
(Hakuna tofauti)

Pitio la 18:37, 3 Aprili 2024

Kiawenti:io Tarbell [1](Alizaliwa Aprili 28)[2][3] Maarufu kwa jina Kiawentiio, ni mwigizaji wa kwanza wa kimataifa ( Mohawk ), mwanamziki na mtunzi wa nyimbo. Alianza kuigiza katika msimu wa tatu wa tamthilia ya CBC series iitwayo Anne with an E (2019) na filamu yake ya kwanza ikiwa Beans (2020) .Aliigiza kama Maya Thomas katika sitcom Rutherford Falls (2021). Alichaguliwa kuigiza kama Katara katika tamthilia ya Avatar: The Last Airbender (2024).

Maisha ya zamani na Elimu

Kiawentiio alizaliwa katika familia ya Mohawk huko Akwesasne, ambayo ni hifadhi ya kwanza ya taifa iliopakana na nchi zote Canada na Marekani na kuzungukwa na mto St Lawrence[4][5]. Kwa upande wa Marekani inajulikana kama hifadhi ya St Regis Mohawk.

Jina lake la kwanza lina maanisha "Asubuhi njema" huko Kanienʼkéha[6]. Wazazi wake ni Barbara na Corey Tarbell. Amekulia katika nyumba ya Kawehno:ke ( pia inajulikana kama Cornwall Island) na kusoma shule ya Uhuru ya Akwesasne na Shule ya Ufundi ya Cornwall Collegiate. Ana uraia wa nchi mbili Canada na Marekani.

Kazi

Tarbell alikuwa mmoja wa waigizaji 200 wenye asili ya Ucanada kwajili ya kuigiza kama Ka'kwet, ambae ameonyeshwa katika msimu wa tatu wa tamthilia ya Anne with an E. Alilazimika kujifunza lugha ya Mi'kmaq na kuelewa utamaduni na historia ya hilo kabila. Pia aligiza katika filamu ya Beans 2020 kama msichana wa Mohawk mwenye umri wa miaka 12 aliekua anaishi Kahnawake mnamo 1990, kipindi cha Mgogoro wa Oka.

Ameonekana kama muhusika wa mara kwa mara akiwa kama Maya Thomas kwenye tamthilia ya Peacock sitcom Rutherford Falls (2021). Pia alichagulia kuvaa uhusika wa Katara katika tamthilia ya Avatar: The Last Airbender series.

Marejeo

  1. https://www.cbc.ca/kidsnews/post/rising-star-meet-kiawentiio-tarbell-new-star-on-anne-with-an-e
  2. "Instagram". www.instagram.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-03.
  3. "Kiawentiio - Actress". TV Insider (kwa American English). 2024-02-22. Iliwekwa mnamo 2024-04-03.
  4. https://www.tribute.ca/people/biography/kiawentiio/59990/
  5. https://www.hitc.com/en-gb/2021/08/13/who-is-kiawentiio-tarbell-explore-the-instagram-ethnicity-and-roles-of-avatar-the-last-airbender-actor/
  6. https://perchmagazine.com/acting-up/