Tantali
Tantali (Tantalum) | |
---|---|
Tantali katika testitubu
| |
Jina la Elementi | Tantali (Tantalum) |
Alama | Ta |
Namba atomia | 73 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 180.94788 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 11, 2 |
Densiti | 8.57 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 3290 K (3017 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 5731 K (5458 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 8 · 10-4 % |
Hali maada | mango |
Tantali ni elementi haba na metali ya mpito yenye namba atomia 73 katika mfumo radidia. Hutokea ndani ya mitapo ya tantaliti.
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Tantali ni metali ngumu yenye rangi ya buluu-kijivu. Tabia zake zafanana sana na Niobi. Tantali tupu inayokaa hewani inapata ganda la oksidi lenye rangi ya kijivu-buluu.
Metali haimenyuki haraka. Chini ya sentigredi 150 haiathiriwi sana hata na asidi. Kiwango cha kuyeyuka cha 3017 °C ni kati ya viwango vya juu kabisa kati ya metali zota pamoja na wolframi na reni.
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Tantali inafaa kwa vyombo vya pekee visivyotakiwa kuwa na kutu au mmenmenyuko kabisa jinsi ilivyo na vyombo vya upasuaji katika tiba lakini pia kwa vipuri vya injini zinazotakiwa kuwa imara kabisa. Matumizi haya yana mipaka yake katika upatikanaji wa tantali na bei yake ya juu.
Sehemu kubwa hutumiwa katika kondensa na resista kwa ajili ya kompyuta na mitambo mingine kwa sababu hapa kiasi kidogo sana kianatosha tayari.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tantali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |