Stuart Chatwood
Stuart Chatwood (alizaliwa 22 Oktoba 1969 Fleetwood, Lancashire, Uingereza) ni mwanamuziki wa nchini Kanada anajulikana kwa upigaji wa kinanda na gitaa aina ya bass kutoka katika bendi ya "The Tea Party". Mnamo mwaka 2001, Chatwood alishinda tuzo ya Juno ikihusisha mchoro bora wa albamu ya Tea Party.
Stuart Chatwood pia ni mtunzi wa vibwagizo vya michezo ya video. Muziki wake umeonekana kwenye vibwagizo vya michezo nane ya tamthilia ikiwemo Prince of Persia iliyoandaliwa na Ubisoft Prince of Persia: The Sands of Time (2003), Warrior Within (2004), The Two Thrones (2005), Battles of Prince of Persia (2005), Revelations (2005), Rival Swords (2007), Prince of Persia (2008), and The Fallen King (2008). Mfululizo huo umefanikiwa kwa kuuza zaidi ya nakala milioni kumi duniani kote. Pia alitunga kibwagizo cha "Darüss Dungeon (2016) na wimbo wake wa Darüss Dungeon II.[1][2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Composer Inon Zur and Stuart Chatwood - Interview at Tracksounds (2008)". Tracksounds.com. Iliwekwa mnamo 2011-07-05.
- ↑ "Stuart Chatwood". MobyGames. Iliwekwa mnamo 2011-07-05.
- ↑ "Ubisoft - Ubisoft Announces Prince Of Persia For Consoles, PC And Nintendo DS". Ubi.com. 2008-04-28. Iliwekwa mnamo 2011-07-05.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Stuart Chatwood kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |