Nenda kwa yaliyomo

Wengu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wengu la binadamu lililotolewa katika maiti.

Wengu (pia "bandama "; kwa Kiingereza spleen, kutoka Kigiriki: σπλήν[1]) ni kiungo cha mwili chenye nafasi katika mzunguko wa damu. Iko ndani ya fumbatio ya mwili karibu na tumbo.

Wengu ya mtu mzima huwa na ukubwa wa takriban sentimita 11 × 7 × 4 na uzito wa gramu 150-200.

Kazi yake ni kuongeza idadi ya seli nyeupe za damu halafu kuondoa seli nyekundu za damu zilizozeeka.

Katika watoto ina pia jukumu la kutengeneza seli nyekundu za damu. Watu wazima kwa kawaida wanaweza kuishi bila wengu.

  1. σπλήν, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wengu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.