Backstreet Boys (wakati mwingine hutajwa kama BSB[1]) ni kundi la uimbaji lililoanzishwa huko mjini Orlando, Florida nchini Marekani mnamo mwaka wa 1993. Kundi hili awali lilikuwa likiunganisha mwimbaji kama vile A. J. McLean, Howie Dorough, Brian Littrell, Nick Carter na Kevin Richardson.

Backstreet Boys

Maelezo ya awali
Asili yake Orlando, Florida, Marekani
Aina ya muziki Pop, pop rock, R&B, teen pop, adult contemporary
Miaka ya kazi 1993–2002, 2005-hadi sasa
Studio Jive, Legacy Recordings
Ame/Wameshirikiana na New Kids on the Block, Elton John
N Sync, Pitbull, Hilary Duff, Nick Lachey, 98 Degrees
Tovuti backstreetboys.com
Wanachama wa sasa
Brian Littrell
Nick Carter
A. J. McLean
Howie Dorough
Kevin Richardson

Wameanza kupata umaarufu wao na albamu yao ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Backstreet Boys (1996). Mwaka uliofuata, wakatoa albamu yao ya pili ya kimataifa, Backstreet's Back (1997) na na albamu yao ya kwanza kutolewa nchini Marekani ambayo iliendelea kulipatia mafanikio kundi hili dunia nzima. Wamekuja kupata umaarufu kupindukia kwa albamu yao ya Millennium (1999) na albamu yake ya kufuatia, Black & Blue (2000).

Baada ya kupumzika kwa miaka mitatu, kundi limejiunga tena na kutoa albamu yao ya marejeo: Never Gone (2005), na vilevile kutoa albamu zingine zaidi kama vile Unbreakable (2007) na This Is Us (2009). Kevin Richardson ameondoka kundini mnamo 2006 ili aweze kuendelea na mambo mengine,[2] lakini alirudi kundi mwaka 2012. The Backstreet Boys wameuza rekodi zaidi ya milioni 130 dunia nzima.[3] Kulingana na Billboard, na kundi la kwanza tangu Sade kuwa na albamu zao za kwanza saba kufikia kumi 10 bora kwenye Billboard 200.[4]

Wanachama

hariri
  • Brian Littrell
  • A.J. McLean
  • Howie Dorough
  • Nick Carter
  • Kevin Richardson

Diskografia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Backstreet Boys". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-02-22. Iliwekwa mnamo 2011-04-12.
  2. "Kevin Richardson Quits Backstreet Boys". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-11-23. Iliwekwa mnamo 2011-11-10.
  3. Garcia, Cathy Rose A.. "Backstreet Boys Share Secrets to Success", The Korea Times, 2010-02-22. Retrieved on 2011-01-24. 
  4. Up for DiscussionPost Comment (2005-07-02). "Never Gone – Backstreet Boys". Billboard.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-22. Iliwekwa mnamo 2009-10-19.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons