Jangwa la Namib
Namib ni jangwa kubwa kwenye pwani la kusini-magharibi ya Afrika hasa nchini Namibia na kusini ya Angola. Eneo lake linaanza kusini kwenye mto Olifants wa Afrika Kusini na huelekea hadi kusini ya Angola. Jina la Namib limetokana na lugha ya Wanama lamaanisha "pasipo na kitu".
Jangwa hili lizunguka eneo ya ukubwa wa takribani kilomita mraba 80,900 [1] (maili mraba 31,200 ). Umbo la Namib ni kanda lenye urefu wa 2000 km na upana wa 100-160 km kuanzia mwambao wa Atlantiki. Jangwa limesababishwa na mkondo wa Benguela unaosukuma maji baridi kutoka Antaktika kuelekea pwani la Afrika. Mkondo huu unazuia mvua kunyesha karibu na mwambao hivyo kuleta hali ya hewa kavu.
Baada ya kustaahimili hali ya ujangwa au nusu jangwa kwa zaidi ya miaka milioni 55[2], inadhaniwa kuwa jangwa kongwe zaidi duniani. Hali ya ukame ya Namib unasababishwa na hewa kavu ya Hadley Cell, inaposhuka na kupoeshwa na hewa ya baridi ya Benguela kando ya pwani. Ina chini ya milimita 10 (nchi 0.4 ) ya mvua kila mwaka na ardhi yake iko karibu tasa.
Kuna spishi kadhaa zisizo za kawaida za mimea na wanyama zinapatikana tu katika jangwa hili. Moja yazo ni Welwitschia mirabilis, moja kati ya spishi zisizo za kawaida. Welwitschia ni mmea unaofanana magugu, lakini inakua tu na majani mawili marefu tu maisha yake yote. Majani haya yanaweza kuwa mita kadhaa kwa urefu, yaliyokunjika na kupindika kutokana na upepo wa jangwani . Mzizi wa kati wa mmea huu hujiendeleza hadi ukawa kama sinia na umri. Welwitschia ni mashuhuri kwa uwezo wake wa kustahimili ukame mkubwa katika jangwa la Namib, wakati mwingine ukitoa unyevu kutoka ukungu wa mwambao.
Namib haina makazi ya watu isipokuwa miji michache pwani. Miji muhimu ni Swakopmund na Walvis Bay penye bandari kuu ya Namibia. Lüderitz ni mji mdogo tu uliokuwa muhimu zaidi zamani za kuchimba almasi karibu na mji huu.
Kuna pia makaazi ya mwaka wote katika eneo la Sesriem, karibu na Sossusvlei iliyo maarufu kutokana namatuta ya mchanga makubwa yanayofikia kimo cha 300m na urefu hadi 30 km, ni miongoni mwa refu zaidi duniani.
Mwingiliano kati ya hewa iliyo jawa na maji kuja kutokea baharini kutoka kwa upepeo wa kusini, baadhi ya upepo ulio na nguvu zaidi kando ya jangwa yoyote kwenye fuo za bahari, na ukame wa hewa ya jangwa husababisha ukungu upepo mkali na kusababisha wanamaji kupoteza njia yao. Pamoja na Pwani ya Skeleton kaskazini zaidi, ina sifa mbaya kama mahali meli hubondeka. Baadhi ya hizi meli zilizobondeka zinaweza kupatikana hata mita 50 barani, huku jangwa likisonga magharibi polepole ndani ya bahari, ardhi keboreshwa itachukua kipindi cha miaka mingi.
Jangwa la Namib ni eneo muhimu kwa ajili ya madini ya Tungsten, chumvi na almasi.
Usafiri ni wa anga kwa kutumia ndege kutoka Windhoek (mji mkuu wa Namibia, karibu kilomita 480 kaskazini-mashariki mwa kituvo cha jangwa), Swakopmund na Walvis Bay kaskazini mwa jangwa, kwa kutumia barabara. Barabara kubwa ya lami kutoka Windhoek kuelekea Swakopmund na nyingine kuelekea Lüderitz zinapita jangwani pamoja na barabara za udongo amabazo zinatunzwa vizuri sana.
Hifadhi ya picha
-
Camel Thorn Tree (Acacia erioloba) katika eneo la Sossusvlei
-
Bahari ya miinuko ya mchanga kwenye Jangwa la Namib. Miinuko ya mchanga imepangika kwa njia ya kaskazini magharibi-kusini mashariki. Miinuko hizi huzuia upepo wa pwani , na kusababisha upepo kubadilisha mwenendo wake kwa kiasi kikubwa kulia , na kwa hivyo kubadili upepo wa kusini kuwa upepo wa kusini mashariki. Eneo wazi iliy kati miinuko ya mchanga na bahari.
-
Lua likitua katika Namib Rand Nature Reserve, Namibia.
-
Picha ya Satellite ya Namib Desert.
-
Jangwa la Namib linavyo onekana kutoka Spot satellite
-
Jangwa la Namib linavyo onekana kutoka Spot satellite
Angalia Pia
- Orodha ya Majangwa kwa eneo
- Animals are Beautiful People, filamu ya asili iliyotungiwa Namib
Marejeo
- ↑ http://www.nationalgeographic.com/wildworld/profiles/terrestrial/at/at1315.html World Wildlife Fund and National Geographic info sheet
- ↑ Namib desert (AT1315), World Wide Fund for Nature site on the Namib Desert
- National Geographic, Januari 1992, pp. 54-85.
- "Dune Patterns, Namib Desert, Namibia". NASA Earth Observatory. Iliwekwa mnamo 2006-05-05.
- Namib Naukluft Park photo gallery
- Namib Desert photo gallery
- Maria Seely: The Namib: Natural History of an Ancient Desert, 3rd ed., Windhoek: Desert Research Foundation ya Namibia 2004, ISBN 99916-68-16-0.