Nenda kwa yaliyomo

Bunge la Umoja wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jengo la Bunge la Umoja wa Afrika

Bunge la Umoja wa Afrika ni mkutano wa wakilishi wa nchi wanachama za Umoja wa Afrika.

Wabunge wake 265 hawapiganiwi kura na raia bali wanateuliwa na bunge za nchi wanachama. Kwa sasa kazi ya bunge ni kushauriana haina mamlaka za kutunga sheria.

Makao ya bunge ndipo mji wa Midrand (Afrika Kusini, sasa kwa muda katika jengo la Gallagher Estate katikati ya Johannesburg na Pretoria. Afrika Kusini inalipa gharama za makao na za ofisi ya bunge.

Mkutano wa kwanza ulitokea Machi 2004. Mwenyekiti wa Bunge ni Gertrude Mongella kutoka Tanzania.

Ana makamu wanne kutoka kanda nne za afrika ndio:

  • F. Jose Dias Van-Du’Nem kutoka Angola (Afrika ya Kusini)
  • Mohammed Lutfi Farhat kutoka Libya (Afrika ya Kaskazini)
  • Loum N. Neloumsei Elise kutoka Chad (Afrika ya Kati)
  • Theophile Nata kutoka Benin (Afrika ya Magharibi)