Nenda kwa yaliyomo

Banjul

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Banjul
Nchi Gambia
Mji Banjul
Wilaya Banjul
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 357 238
Muonekano wa Mji wa Banjul
Mahali pa Banjul katika Gambia
Banjul mjini
Geti ya Arch 22 ya kuingia mji wa Banjul

Banjul ni mji mkuu wa Gambia. Mji wenyewe una wakazi 34,828 pekee[1] lakini pamoja na mitaa ya nje ni zaidi ya nusu milioni.

Banjul iko kwenye kisiwa cha Mt. Mariamu (au: Kisiwa cha Banjul) mdomoni mwa mto Gambia unapoishia katika bahari ya Atlantiki.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Waingereza walianzisha mji mwaka 1816 BK kama kituo cha biashara na kituo cha kijeshi cha kukomesha biashara ya watumwa. Jina la mji lilikuwa "Bathurst" kufuatana na Henry Bathurst aliyekuwa waziri wa makoloni wakati ule.

Mwaka 1965 Bathurst ilikuwa mji mkuu wa nchi huru ya Gambia. Mwaka 1973 jina lilibadilishwa kuwa Banjul. Tarehe 22 Julai 1994 palikuwa na mapinduzi wa kijeshi yaliyoanzisha utawala wa Rais Yahaya Jammeh. Geti la mji "Arch 22" lilijengwa kama kumbukumbu ya mapinduzi haya.

Banjul ni kitovu cha utawala na biashara katika Gambia.

Mawasiliano ndani ya nchi ni hasa kwa njia ya feri kwenye mto Gambia hadi mji wa Barra.

Msingi wa uchumi ni kilimo, hasa karanga, nta, mawese na ngozi zinasafirishwa kutoka bandari ya Banjul.

Banjul ina uwanja wa ndege wa kimataifa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Wakazi ya Infobox - Statoids, Gambia Divisions, 2003, see Banjul Division (Kiingereza)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Banjul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.