Fibonacci
Mandhari
Fibonacci (mnamo 1175 - 1250) alikuwa mtaalamu wa hisabati kutoka nchini Italia. Anakumbukwa kama mwanahisabati muhimu zaidi wa Ulaya wakati ya zama za kati.
Jina lake la kiraia ilikuwa Leonardo wa Pisa lakini aliitwa kwa jina la baba yake Bonacci.
Mfululizo wa Fibonacci
[hariri | hariri chanzo]Fibonacci anakumbukwa hasa kwa jedwali la namba linaloitwa mfululizo wa Fibonacci.
Linaanza hivi: 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21, 34, 55, 89, ...
Katika mfululizo huu namba inayofuata ni jumla ya namba mbili zinazotangulia:
1 + 1 = 2 1 + 2 = 3 2 + 3 = 5 3 + 5 = 8 5 + 8 = 13 8 + 13 = 21 13 + 21 = 34 21 + 34 = 55 34 + 55 = 89 55 + 89 = 144 89 + 144 = 233 144 + 233 = 377 233 + 377 = 610 377 + 610 = 987 610 + 987 = 1597 987 + 1597 = 2584 na kadhalika...