Nenda kwa yaliyomo

Hidrati kabonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kabohidrati)

Hidrati kabonia (pia: kabohidrati au hamirojo) ni kampaundi ya kikemia inayojengwa kwa oksijeni, hidrojeni na kaboni. Katika kemia huitwa kwa jumla kwa jina "sukari" hata kama sukari kwa lugha ya kawaida ni sehemu tu ya kabohidrati.

Hidrati kabonia ni kati ya molekyuli muhimu zinazojenga viumbehai duniani. Kazi zake ni nyingi: kwa mfano, kuhifadhi na kubeba nishati (wanga) ndani ya mwili wa wanyama na mimea au kujenga mwili kwa umbo la selulosi au chitini cha wadudu.

Umbo la msingi wa kabohidrati ni monosakaridi (Cn(H2O)n) zinazoungana kuwa aina nyingine za kabohidrati.

Aina za hidrati kabonia ni kwa mfano:

Hidrati kabonia ni chanzo cha nishati katika chakula cha watu wengi. Takriban asilimia 40 - 75 za mahitaji ya nishati ya watu hutokana na hidrati kabonia. Vyakula vyenye hidrati kabonia nyingi ni vile vyenye wanga, hasa nafaka, na vyote vilivyotengenezwa kwa kutumia nafaka kama vile ugali, mkate, pasta, wali pamoja na mazao kama viazi na ndizi.

Vyakula hivyo tofauti vina viwango tofauti vya hidrati kabonia: vyakula kama vilivyoundwa viwandani kama vile sukari, mkate na pasta vikiongoza vikifuatwa na nafaka zilizosagwa. Vyakula kama vile nafaka vinavyopikwa bila kusagwa zina viwango vya chini vya hidrati kabonia. Hivyo ni muhimu, hasa kwa walio na magonjwa kama vile ya kisukari[1] au hali za kimwili kama vile wanariadha[2], wanaohitaji viwango fulani cha nichati, kuwa wangalifu na ikiwezekana kupima viwango vya hidrati kabonia katika vyakula vyao. Kuna njia tofauti za kuhesabu hidrati kabonia katika chakula, ikiwemo vikokotoo vilivyo mitandaoni[3][4].

Katika tamaduni chache watu hula kabohidrati kidogo na karibu chakula chote ni protini ya nyama, kama vile kati ya Eskimo au Wamasai wanaokula hasa protini, lakini mwili unaweza kubadilisha protini kuwa kabohidrati isipokuwa lishe yake inapungua.

  1. "Chapter 3 - Dietary carbohydrate and disease". www.fao.org. Iliwekwa mnamo 2019-05-17.
  2. Kanter, Mitch (2018-1). "High-Quality Carbohydrates and Physical Performance". Nutrition Today. 53 (1): 35–39. doi:10.1097/NT.0000000000000238. ISSN 0029-666X. PMC PMCPMC5794245. PMID 29449746. {{cite journal}}: Check |pmc= value (help); Check date values in: |date= (help)
  3. "CHAPTER 3: CALCULATION OF THE ENERGY CONTENT OF FOODS - ENERGY CONVERSION FACTORS". www.fao.org. Iliwekwa mnamo 2019-05-17.
  4. "Net Carbs Calculator". Calculator Academy (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-05-17.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hidrati kabonia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.