Kampala
Jiji la Kampala | |
Mahali pa mji wa Kampala katika Uganda |
|
Majiranukta: 0°18′49″N 32°34′52″E / 0.31361°N 32.58111°E | |
Nchi | Uganda |
---|---|
Wilaya | Kampala |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 1 353 236 |
Tovuti: www.kcc.go.ug |
Kampala ni mji mkuu wa Uganda, pia mojawapo ya wilaya za nchi. Iko karibu na ziwa kubwa la Nyanza Viktoria, mita kama 1,189 juu ya UB.
Kampala ni mji mkubwa wa Uganda ikiwa na wakazi 1,208,544 (2002).
UNDIO, UNEP, Benki ya Uchumi na East Africa Development Bank (EADB) zina ofisi hapa.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la Kampala limetokana na msemo wa Kiganda "Kasozi K'Empala" wenye maana ya "kilima cha swala" kwa sababu wafalme wa Buganda walipenda kuwinda katika eneo hili.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kampala ni mji ulioanza kukua sehemu za vilima mbalimbali upande wa kaskazini wa Entebbe.
Kitovu cha kwanza kilikuwa nyumba ya kifalme kwenye kilima cha Kasubi iliyojengwa na Kabaka Mutesa I wa Buganda mnamo mwaka 1882. Baada ya kifo chake Mutesa ikawa kaburi la kifalme. Ikulu mpya ya Kabaka Mwanga II ikajengwa karibu kwenye kilima cha Mengo.
Mwaka 1890 mwakilishi wa Kampuni ya Kifalme ya Uingereza kwa Afrika ya Mashariki (IBEA, kifupi kwa Imperial British East Africa Company), Frederick Lugard aliingilia vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Waganda Waprotestanti, Wakatoliki na Waislamu, akajenga boma juu ya kilima kilichoitwa "Kampala" kikawa kitovu cha makao ya Wazungu katika mji mpya.
Wamisionari wakapewa na Kabaka nafasi ya kujenga makanisa na nyumba zao kwenye vilima mbalimbali: Namirembe ikawa kilima cha Waanglikana, Rubaga kilima cha Wakatoliki. Waislamu walikuwa na eneo lao hasa kwenye kilima cha Kibuli.
Maeneo hayo yote yaliunganika pamoja kuwa mji wa Kampala.
Kati ya 1900 hadi 1905 Kampala ikawa makao makuu ya utawala wa kikoloni wa Uingereza uliohamishwa baadaye kwenda Entebbe.
Baada ya uhuru ikawa mji mkuu wa kitaifa wa Uganda.
Utawala wa Idi Amin na vita vya kumpindua 1979 uliharibu mengi, kwanza tabaka la wafanyabiashara Wahindi pamoja na nguvu ya kiuchumi, baadaye pia majengo.
Tangu kufufuka kutoka nyakati mbaya za udikteta na vita, Kampala imeanza kukua tena.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Wakazi |
---|---|
Sensa 1959 | 46.000 |
Sensa 1980 | 458.503 |
Sensa 1991 | 774.241 |
Sensa 2002 | 1.208.544 |
Sensa 2005 | 1.353.236 |
Makadirio 2015 | 1.803.936 |
Makerere
[hariri | hariri chanzo]Kampala ina Chuo Kikuu katika mtaa wa Makerere kilichokuwa chuo kikuu cha kwanza katika Afrika ya Mashariki na mahali pa mafunzo kwa viongozi wengi wa Kiafrika upande wa siasa, utamaduni na uchumi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Archived 12 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Uganda bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kampala kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |