Karim Benzema
Karim Mostafa Benzema (alizaliwa Lyon, 19 Desemba 1987) ni mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa. Anajulikana kama mshambuliaji mwenye kipaji na nguvu.
Maisha ya klabu
[hariri | hariri chanzo]Kipindi cha awali
[hariri | hariri chanzo]Benzema alianza uchezaji kwenye klabu ya Terraillon akiwa na umri wa miaka 8,katika miaka ya 1990, viongozi wa Lyon walikuwa walimtembelea moja kwa moja katika swali la kumsaini kijana huyo.
Lyon
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuzungumza na babake Benzema, klabu hiyo ilimruhusu mchezaji huyo kufanyiwa majaribio na Lyon. Kufuatia majaribio hayo, Benzema alijiunga rasmi na Lyon na kuingizwa katika akademi ya klabu hiyo. Kwenye msimu wa 2004-2005 aliiwezesha timu yake kushinda makombe matatu,na msimu wa 2007-08 alibeba kombe la ligi na kuwa kombe la saba kwa Olympique Lyonnais, na kuwa mchezaji bora wa mwaka,na kuwa timu bora ya mwaka.Benzema alikuwa mfungaji bora na kushinda tuzo kutoka gazeti la Italia la Guerin Sportivo. Msimu uliofuata Olympique Lyonnais ilimuuza kwenda Real Madrid kwa ada ya £35 milioni ($50 milioni)na kusaini miaka sita. [1]
Real Madrid
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuhangaika ili aweke heshima, kwa misimu miwili alishinda magoli 32 na kuiwezesha Real Madrid kushinda Copa Del Rey mwaka 2011, na msimu wa 2011-12 alikuwa mchezaji bora mfaransa mara tatu mwaka 2011,2012,2014.[2]
Mnamo Oktoba 2021, katika kesi ya ngono ya Mathieu Valbuena, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Versailles iliomba korti ya jinai kumpa adhabu ya kifungo cha miezi kumi kilichosimamishwa na faini ya euro 75,000.
Mashtaka ya 2023
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Oktoba 2023, Benzema alionyesha mshikamano na waathiriwa wa mashambulio ya anga ya Israeli huko Gaza. Kujibu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gérald Darmanin alimshutumu Karim Benzema kwa "kuwa na uhusiano" na kundi linalojulikana kama Muslim Brotherhood. Naye seneta kutoka chama cha Republican cha Bouches-du-Rhône, Valérie Boyer, alitaka mchezaji huyo anyimwe uraia wa Ufaransa na Ballon d'Or iwapo mashtaka yatathibitishwa.[3]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Benzema va signer Olympique Lyonnais Reserve Pro: Saison Football 2004/2005", Stat2Foot. (fr)
- ↑ "Forward Benzema joins Real Madrid from Lyon". ESPN. 1 Julai 2009. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "POLITIQUE ISLAM Gérald Darmanin lie Karim Benzema aux Frères musulmans, le Ballon d'or envisage de porter plainte". Le Monde. 19 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2023.
{{cite web}}
: line feed character in|title=
at position 10 (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Karim Benzema kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |