Nenda kwa yaliyomo

Kate Maki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kate Maki.

Kate Maki ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka Kanada.[1][2]

Biografia

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa na kukulia Sudbury, Ontario, Maki amesomea sayansi ya neva katika chuo cha Dalhousie huko Halifax, Nova Scotia na ualimu katika Nipissing University huko North Bay Ontario.[3] Alifundisha elimu maalum, Kifaransa na sayansi huko Ottawa, Toronto na Sudbury kwa miaka kabla hajaamua kufanya kazi ya muziki kwa wakati wote.[4]

Mnamo 2003, Maki alirekodi albamu yake ya kwanza, Confusion Unlimited, pamoja na Dave Draves katika studio za Bullhorn huko Ottawa, Ontario.[5] Mnamo 2004, alirudi katika studio za Little Bullhorn na kurekodi albamu yake ya pili, The Sun Will Find Us. Albamu zote zilipata Tuzo za Albamu ya Mwaka katika Muziki wa Ontario ya Kaskazini na Tuzo za Filamu mwaka 2004 na 2005.

Mnamo 2005, Maki, Nathan Lawr, Ryan Bishops, Ruth Minnikin na Dale Murray walishiriki ziara mbili za matamasha ya kitaifa, A Midautumn Night’s Dream na A Midwinter Night’s Dream, ambayo ilisemwa kuongozwa na Rolling Thunder Revue ya Bob Dylan. Wanamuziki watano pia walirekodi matoleo madogo ya mkusanyiko wa kila ziara yao.

Maki alipumzika kufanya ziara kati ya miaka 2006 na 2008 na kurejea nyumbani Sudbury, Ontario kufundisha sekondari sayansi. Wakati wa mapumziko Machi 2007, Maki alirekodi albamu yake ya tatu, On High, katika studio za Little Bullhorn pamoja na Howe Gelb kama mtayarishaji na Dave Draves kama mkandarasi.[6] Ilitolewa Marekani ya Kaskazini mnamo Februari 12, 2008, na alitunukiwa Albamu ya Mwaka katika Muziki wa Ontario ya Kaskazini na Tuzo za Filamu mwaka 2009.

Marekani

[hariri | hariri chanzo]

Wakati akifanya ziara Marekani mwaka 2008, Maki alisimama WaveLab huko Tucson, Arizon kwa siku mbili kurekodi albamu yake ya nne, Two Song Wedding, ambayo ilitolewa Januari 2010.[7]

Mwishoni mwa 2010, Maki na Mkanada mwenzake Fredrick Squire walisafi kwenda kwenye studio za Paco Loco huko El Puerto de Santa Maria kurekodi nyimbo mbili za country. Calling it Quits/Crazy Tropical Survival Guide ulitolewa kama wimbo wa inchi - saba - wenye nyimbo mbili na kupakua kidigitali mnamo Machi 22, 2011.

Baada ya kufanya ziara Kanada pamoja mwaka 2011 kuunga mkono albamu yao ya inchi - saba na vile vile albamu binafsi ya tano ya Maki, Moonshine na albamu binafsi ya pili ya Squire, Frederick Squire Sings Shenandoah and Other Popular Hits , wawili hao waliamua kupumzika kufanya ziara na kukaa Copper Cliff, Ontario kuanzisha familia. Squire na Maki walioana mnamo Decimba 22, 2012. Albamu ya Maki ya hivi karibuni, Head in the Sand, ilitolewa mnamo Mei 2016.[8]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Confusion Unlimited (2003)
  • The Sun Will Find Us (2004)
  • On High (2008)
  • Two Song Wedding (2010)
  • Moonshine (2011)
  • Head in the Sand (2016)

Mikusanyiko ya kwenye Ziara

[hariri | hariri chanzo]
  • A Midwinter Night's Dream (2005)
  • A Midautumn Night's Dream (2005)
  • Calling It Quits/Crazy Tropical Survival Guide (2011, pamoja na Frederick Squire)

Kama Mwanamuziki Mgeni

[hariri | hariri chanzo]
  • sauti: "Cocaine Cowgirl" na "St. George's Lane" - Matt Mays - Matt Mays + El Torpedo (albamu) (2004)
  • sauti/gitaa la umeme: "Covering Up" - Nathan Lawr - Secret Carpentry (2005)
  • sauti: "Mountain of Love" - Howe Gelb - Sno Angel Like You (2006)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]