Kaunti ya West Pokot
Kaunti ya West Pokot | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
Wanawake Wapokot wakiwa Kapenguria, Pokot Magharibi | |||||
| |||||
West Pokot County in Kenya.svg Kaunti ya West Pokot katika Kenya | |||||
Coordinates: 1°14′00″N 35°07′00″E / 01.23333°N 035.1167°E | |||||
Nchi | Kenya | ||||
Namba | 24 | ||||
Ilianzishwa | March 4, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Bonde la Ufa | ||||
Makao Makuu | Kapenguria | ||||
Gavana | Prof. John Krop Lonyangapuo | ||||
Naibu wa Gavana | Dkt. Nicholas Owon Atudonyang | ||||
Seneta | Samuel Losuron Poghisio | ||||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Lilian Tomitom | ||||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya West Pokot | ||||
Spika | Catherine Mukenyang | ||||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 20 | ||||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 | ||||
Eneo | km2 9 123.2 (sq mi 3 522.5) | ||||
Idadi ya watu | 621,241 | ||||
Wiani wa idadi ya watu | 68 | ||||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti | http://westpokot.go.ke |
Kaunti ya West Pokot ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 621,241 katika eneo la km2 9,123.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 68 kwa kilometa mraba[1]..
Makao makuu yako Kapenguria.
Inajulikana kwa kuwa na bwawa la uzalishaji umeme la pekee lililo kaskazini mwa Bonde la Ufa liitwalo Turkwell. Pia, Makumbusho ya Kapenguria yapo katika kaunti hii, ambapo wapigania uhuru sita walikamatwa na kufungwa jela na serikali ya kikoloni wakati wa hali ya hatari mwaka 1952.
Jiografia
Kaunti ya Pokot Magharibi ina eneo la ukubwa wa km2 9 169.4 (sq mi 3 540.3). Imepakana na Uganda (magharibi), Turkana (kaskazini), Trans Nzoia na Elgeyo Marakwet (kusini) na Baringo (kusini mashariki).
Kaunti hii ina tabianchi kavu na nusu kavu. Kiwango cha mvua ni kati ya mm 400 hadi mm 1500 kila mwaka. Halijoto huwa kati ya 10 °C na 30 °C[2].
Maeneo bunge
Kaunti ya Pokot Magharibi ina maeneo bunge yafuatayo[3]:
Eneo bunge | Kata |
---|---|
Kapenguria | Riwo, Kapenguria, Mnagei, Siyoi, Endugh, Sook |
Sigor | Sekerr, Masool, Lomut, Weiwei |
Kacheliba | Suam, Kodich, Kasei, Kapchok, Kiwawa, Alale |
Pokot South | Chepareria, Batei, Lelan, Tapach |
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]
- Kipkomo 102,633
- Pokot Central 119,016
- Pokot North 134,485
- Pokot South 80,661
- West Pokot 184,446
Tazama pia
Marejeo
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ "West Pokot". www.crakenya.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-29. Iliwekwa mnamo 2018-08-05.
- ↑ "West Pokot County | County Trak Kenya". countytrak.infotrakresearch.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-08-05.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya West Pokot kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |