Nenda kwa yaliyomo

Mahikeng

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahikeng, South Afrika


Jiji la Mahikeng
Jiji la Mahikeng is located in Afrika Kusini
Jiji la Mahikeng
Jiji la Mahikeng

Mahali pa mji wa Mahikeng katika Afrika Kusini

Majiranukta: 25°49′48″S 25°36′36″E / 25.83000°S 25.61000°E / -25.83000; 25.61000
Nchi Afrika Kusini
Majimbo Kaskazini-Magharibi

Mahikeng ni jina la mji mkuu wa jimbo la Kaskazini-Magharibi la Afrika Kusini. Siku hizi mji uliunganishwa na mji jirani wa Mmabatho na kuhesabiwa kama sehemu yake.

Mafeking ilianzishwa na Waingereza waliopewa hapa ardhi na chifu wa Barolong. Jina latokana na lugha ya KiTswana likimanisha "mahali pa mawe".

Wakati wa Vita ya pili ya Waingereza dhidi ya Makaburu mji ulizungushwa na jeshi la makaburu lakini ulitetewa na Robert Baden-Powell aliyeanzisha baadaye harakati ya maskauti.

Kati ya 1894 hadi 1965 mji ulikuwa makao makuu ya utawala wa Bechuanaland (Botswana ya leo).

Wakati wa siasa za bantustan Mafeking ilikuwa pia mji mkuu wa Bophuthatswana lakini serikali yake ilihamishwa baadaye kwenda mji jirani wa Mmabatho uliokuwa kwenye eneo la bantustan.

Mwaka 1994 Mahikeng na Mmabatho ziliunganishwa kiutawala na kuwa mji mkuu wa jimbo jipya la Kaskazini-Magharibi linalounganisha maeneo ya majimbo ya awali ya Transvaal na Rasi (Cape) pamoja na sehemu kubwa ya bantustan ya Bophuthatswana.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mahikeng kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.