Mariam Baouardy
Mariam Baouardy (kwa Kiarabu: مريم بواردي; jina la kitawa: Mariamu wa Yesu Msulubiwa; I’billin, Palestina, 5 Januari 1846 – Bethlehemu, Israeli, 26 Agosti 1878) alikuwa mmonaki wa Kanisa Katoliki la Kimelkiti katika shirika la Wakarmeli Peku.[1].
Baada ya kufiwa wazazi alihamia Aleksandria, Misri, alipoteswa na ndugu ya baba yake kwa kukataa kuolewa akachanwa koo na Mwislamu fulani kwa kukataa kusilimu, alinusurika kufa kwa msaada wa Bikira Maria, ila sauti haikutoka tena sawasawa hadi mwisho wa maisha yake[2]. Baadaye alipatwa na upofu akabaki hivyo siku 40, kisha akapona ghafla.
Pamoja na kuhudumia maskini kwa upendo alijulikana kwa karama zake za pekee, yakiwemo madonda matano ya Yesu mwilini mwake[3].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Novemba 1983, Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 17 Mei 2015.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ dauplay. "Sa Vie". carmel.asso.fr. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Maram Baouardy", Melkite Eparchy of Newton
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90045
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |