Mpasua mbao
Mandhari
Mpasua mbao ni mtu ambaye kazi yake ni kukata miti na kuipasua kwa matumizi ya mbao na kuni.
Katika historia kazi hiyo ilitekelezwa mwanzoni na mtu yeyote. Katika jamii zilizojenga tasnia kubwa kama vile uchimbaji wa madini, ufuaji metali na ujenzi wa jahazi, upasuaji wa ubao uliendelea kuwa kazi ya pekee iliyohitaji maarifa na vifaa maalumu ili kutosheleza mahitaji ya tasnia hizo.
Upasuaji wa mbao ni kazi ngumu na hatarishi iliyotekelezwa kwa karne nyingi kwa zana kama shoka na msumeno. Tangu karne ya 20 vifaa vipya vinavyoendeshwa kwa injini kama msumeno wa mnyororo vimepatikana. Leo hii ni kawaida mpasua mbao kuwa pia na nguzo kumkinga dhidi ya jeraha na sauti kubwa ya injini.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mpasua mbao kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |