Nenda kwa yaliyomo

Ncha ya kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ncha ya Kusini na Ncha Sumaku

Ncha ya kusini ni mahali pa kusini kabisa duniani. Neno hili hutaja ama

  • ncha ya kijiografia ya kusini au
  • ncha sumaku ya kusini.

Duniani iko kinyume cha ncha ya kaskazini.

Ncha ya kusini ya Kijiografia

[hariri | hariri chanzo]

Ncha ya kusini ya kijiografia iko katikati ya bara la Antaktiki. Ni mahali ambako mhimili wa kuzunguka kwa dunia unagusa uso wa dunia. Mahali hapa papo kwa anwani ya kijiografia ya 90°S na 0°W takriban 2,800 m juu ya UB. Uso wa dunia umefunikwa hapa na ganda nene la barafu lenya upana wa mita 2,700 kwa hiyo uso wa dunia mwenyewe uko kidogo tu juu ya UB.

Mazingira ya ncha ni baridi sana. Antaktika yote hakuna wakazi wa kudumu bali wanasayansi wa mataifa mbalimbali katika vituo vya utafiti. Papo hapo nchani kuna kituo cha Kimarekani kinachoitwa "Amundsen-Scott South Pole Station" penye wanasayansi pamoja na wataalamu 100 - 200. Idadi inategemea na majira, ni wengi wakati wa mchana na wachache wakati wa usiku.

Usiku na mchana ina muda wa nusu mwaka. Macheo ya pekee hutokea kila mwaka tar. 21 Septemba na mchana unaendelea hadi 21 Machi siku ya machweo. Giza inaanza na usiku huendelea hadi Septemba.

Ncha sumaku ya kusini

[hariri | hariri chanzo]

Ncha ya kuzunguka dunia si sawa na ncha sumaku yaani mahali panapoonyeshwa na sumaku za dira dunia. Hapa ni kitovu cha kusini cha ugasumaku wa dunia.

Ncha sumaku hutembeatembea kama mwenzake huko kaskazini. Kwa sasa iko nje ya Antaktika lakini iko tofauti kila mwaka.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Watu wa kwanza wa kufikia ncha ya kusini tar. 14 Desemba 1911 walikuwa Roald Amundsen na wenzake kwa jumla kundi la Wanorwei 5. Walitangulia mbele ya kundi la Robert F. Scott waliofika nyuma yao tar. 17 / 18 Januari 1912 nchani lakini walikufa shauri ya njaa na baridi wakati wa kurudi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]