Nenda kwa yaliyomo

Pigo la kona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ikionyesha kona ikipigwa na timu iliyovaa jezi za rangi ya bluu na nyeupe.
Alessandro Del Piero wa klabu ya Sydney F.C. akipiga kona.

Pigo la kona ni aina ya uanzishaji wa mpira uliokufa baada ya mpira kutoka nje ya uwanja kwa kuvuka mstari wa upande wa goli bila ya goli kufungwa na mpira huo kuwa umeguswa na mchezaji wa timu inayokaba. Mpira hupigwa kwa kutengwa kwenye kona ya uwanja, mahali mstari wa pembeni unapokutana na mstari wa upande wa goli. Mara kadhaa upigaji wa kona huweza kusababisha goli lakini ni nadra kulinganisha na penalti au faulu zinazopigwa karibu na eneo la penalti.

Utaratibu

[hariri | hariri chanzo]
Mchezaji akiwa anapiga kona.
  • Refa msaidizi hutoa ishara ya kona kwa kunyoosha bendera juu na kuelekeza eneo la kona, hata na hivyo hii haimaanishi atakaponyooshea bendera ndipo kona itakapo pigiwa, refa ndiye anayetoa maamuzi kwa kunyoosha mkono kuelekeza eneo la kupigia. Refa huonyesha eneo la kupigia kona kwa kunyoosha mkono juu kuelekea upande wa kupigia kona.
  • Mpira lazima uwekwe chini katika eneo lililochorwa robo duara lenye nusu kipenyo cha mita moja kutoka kwenye bendera ya kona maalumu kwa ajili ya kupiga kona.[1][2]
  • Wachezaji wote ambao kona inaelekezwa golini kwao lazima wawe umbali wa mita 9 kutoka kona inapopigiwa mpaka kona itakapopigwa, kama watahitaji kukaba kona itakayoanzishwa kwa pasi fupi, itawalazimu kusimama umbali huo katika alama zilizowekwa kwenye mstari wa pembeni na ule wa upande wa goli. [3]
  • Mpira utakua umeanzishwa ukipigwa na ukasogea bila ya utatanishi wowote, sio lazima uvuke eneo la kona.[1]
  • Mchezaji anayepiga kona hawezi kugusa mpira mara mbili au zaidi kabla mchezaji mwingine hajaugusa.[1]
  • Timu inayoshambulia inaweza kufunga goli kwa kupiga kona moja kwa moja (japo ni nadra sana. Goli la kujifunga haliwezi kutokea kwa timu inayoshambulia, katiak hali isiyo ya kawaida mpira ukipigwa ukaenda moja kwa moja na kuingia katika goli la aliyepiga haiwezi kuhesabiwa kama goli bali itakua kona itakayoelekezwa golini kwake.
  • Mchezaji yoyote anayeshambulia hawezi kuitiwa kosa la kuotea endapo atapokea mpira moja kwa moja kutoka kwa mpiga kona.

Uvunjwaji sheria

[hariri | hariri chanzo]

Kona ikipigwa mpira ukiwa unasogea au eneo lisilo sahihi, basi italazimika kurudia kupiga kona hiyo.[4]

Wachezaji wanaokaba ni lazima wawe umbali unaotakiwa kisheria kama ilivyoelezewa hapo juu, kutofuata sheria hiyo kunaweza kusababisha adhabu ya faulu au kuonyeshwa kadi ya njano.[5]

Ni kosa kwa mchezaji anayepiga kona kugusa mpira kwa mara ya pili kabla mchezaji mwingine uwanjani hajaugusa mpira. Kosa hili huadhibiwa timu kupigiwa faulu isiyo ya moja kwa moja kutoka eneo alipogusia mpira,[6] vinginevyo katika kugusa mpira kwa mara ya pili mchezaji aliushika, hapa faulu ya moja kwa moja itapigwa kuelekeza golini kwake.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Laws of the Game: Law 17: Corner Kick: Procedure". 2019. Iliwekwa mnamo 2019-09-22.
  2. "Laws of the Game: Law 1: The Field of Play: The Corner Area". 2019. Iliwekwa mnamo 2019-09-22.
  3. "Laws of the Game: Law 1: The Field of Play: Field Markings". 2019. Iliwekwa mnamo 2019-09-22.
  4. 4.0 4.1 "Laws of the Game: Law 17: Corner Kick: Offences and Sanctions". 2019. Iliwekwa mnamo 2019-09-22.
  5. "Laws of the Game: Law 12: Fouls and Misconduct: Disciplinary Action". 2019. Iliwekwa mnamo 2019-09-22.
  6. Law 17 - The corner kick Archived 29 Desemba 2014 at the Wayback Machine., Laws of the game on FIFA.com (Archive, 10 April 2014)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Pigo la kona kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.