Saint Jhn
Carlos St. John (anavyojulikana zaidi kwa jina la usanii kama Saint Jhn, inavyoandikwa kimtindo kama SAINt JHN), ni rapa, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki mwenye asili ya Kiguyana na Kimarekani. Aliachia albamu yake ya kwanza chini ya jina la kisanii Saint Jhn, Collection One, mnamo Machi 2018. Kabla ya hapo, Jhn aliandikia nyimbo wasanii kadhaa akiwemo Jidenna, Hoodie Allen, Usher, Kiesza, na wengineo. Yeye ni mwanachama mwanzilishi wa kundi la muziki la GØDD COMPLEXx.
Maisha ya mwanzoni
[hariri | hariri chanzo]Carlos St John alizaliwa Brooklyn, New York. Aligawanya wakati wake kati ya Brooklyn na Guyana katika ukuaji wake. Alianza kuunda muziki wakati akiwa mwenye umri mdogo wa miaka 12 na aliongozwa na kaka yake mkubwa, ambaye aliimba katika ujirani wake na marafiki. Aliandika wimbo wake wa kwanza katika mwaka wake wa kwanza wa shule ya upili alipokuwa akiishi nchini Guyana.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya kupitisha jina la kisanii la Saint Jhn, aliimba na kutunga nyimbo kwa kutumia jina lake la kuzaliwa, Carlos St. John (au Carlos Saint John). Mnamo mwaka wa 2010, aliachilia EP ya (The St. John Portfolio) na mixtape (In Association) chini ya jina lake la kuzaliwa. Mara tu baada ya hapo, alipeperushwa kwa ndege hadi Los Angeles na msimamizi wa muziki, Zach Katz. Kwa muda wa miezi miwili, alimuandikia nyimbo Rihanna, lakini hakuna wimbo hata mmoja uliokubalika. Baada ya kurudi nyumbani, Jhn aliandika wimbo wa Hoodie Allen wa 2012, "No Interruption."
Katika miaka iliyofuata, Jhn aliwaandikia nyimbo Kiesza, Gorgon City na Nico & Vinz miongoni mwa wengineo. Mnamo mwaka wa 2016, alipata utambuzi wa mtunzi wa nyimbo kwa nyimbo za Usher, "Crash" na "Rivals," zote mbili zikitokea kwenye albamu ya Hard II Love. Pia mnamo 2016, aliachia wimbo wake wa kwanza chini ya jina lake la usanii, Saint Jhn, ulioitwa "1999." Aliufuatilia na nyimbo zingine mbili mnamo 2016, "Roses" na "Reflex." Mnamo Oktoba 2016, ilitangazwa kuwa JHN atamfungulia kumbi Post Malone wakati wa msururu wa maonyesho kwenye Pwani ya Magharibi Marekani.
Mnamo Februari 2017, Albamu ya Jidenna>, The Chief, ilitolewa ambayo iliyokuwa na wimbo wa "Helicopters / Beware" ambapo Jhn alikuwa mtunzi mwenza. Mwezi uliofuata, Jhn aliachilia wimbo mwingine halisi, "3 Below." Mnamo Oktoba wa mwaka huo, alitumbuiza kwenye sherehe mbili, Rolling Loud na Voodoo Experience. Pia aliachia wimbo mwingine mpya, "Hermes Freestyle." Mnamo Februari 2018, Jhn aliachilia "I Heard You Got Too Litt Last Night." Mwanzoni mwa Machi, aliachia wimbo, "Albino Blue ", na Machi 30, 2018, albamu yake ya kwanza ilitolewa. Wakati huo, nyimbo zilizokuwa zimetolewa tayari kwenye albamu hiyo zilikuwa zimekusanya jumla ya utazamaji na usikilizaji milioni 50 kwenye majukwaa kadhaa ya mtandao. Mbali na kufanya kazi kwenye muziki na safari ya kuunga mkono Collection One, Jhn aliajiriwa na kampuni ya Gucci kama model wa kampeni ya Gucci iliyoitwa "Guilty" akiambishwa na Adesuwa Aighewi.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu za studio
[hariri | hariri chanzo]Kichwa | Maelezo | Nafasi za chati ya Peak | |
---|---|---|---|
US |
CAN | ||
Collection One |
|
— | — |
Ghetto Lenny's Love Songs |
|
39 | 41 |
EPs
[hariri | hariri chanzo]Kichwa | Maelezo |
---|---|
The St. John Portfolio(as Carlos St. John) |
|
Mixtapes
[hariri | hariri chanzo]Kichwa | Maelezo |
---|---|
In Association(as Carlos St. John) |
|
Singles
[hariri | hariri chanzo]Kama msanii mkuu
[hariri | hariri chanzo]Jina | Mwaka | Nafasi za chati ya Peak | Albamu | |||
---|---|---|---|---|---|---|
US | CAN | NLD | UK | |||
"1999" | 2016 | — | — | — | — | Non-album single |
"Some Nights" | 2017 | — | — | — | — | Collection One |
"N***a Sh*t (Swoosh)" | 2018 | — | — | — | — | |
"McDonalds Rich" | — | — | — | — | Non-album singles | |
"White Parents Are Gonna Hate This" | — | — | — | — | ||
"Trap"
(featuring Lil Baby) |
2019 | — | — | — | — | Ghetto Lenny's Love Songs |
"Brown Skin Girl"
(with Beyoncé and Wizkid featuring Blue Ivy Carter) |
76 | 60 | 82 | 42 | The Lion King: The Gift | |
"Anything Can Happen"
(featuring Meek Mill) |
— | — | — | — | Ghetto Lenny's Love Songs |
Kama msanii aliyeshirikishwa[edit]
[hariri | hariri chanzo]Jina | Mwaka | Albamu |
---|---|---|
"Beretta Lake"
(Teflon Sega featuring Saint Jhn) |
2016 | Non-album single |
Utunzi na utayarishaji
[hariri | hariri chanzo]Jina la wimbo | Mwaka | Wasanii wakuu | Albamu | Jukumu |
---|---|---|---|---|
"No Interruption" | 2012 | Hoodie Allen | All American | Mtunzi mwenza |
"Bad Thing" | 2014 | Kiesza | Sound of a Woman | |
"The Love" | ||||
"Piano" | ||||
"Praying to a God" | 2015 | Nico & Vinz | Cornerstone | |
"Doubts" | 2016 | Gorgon City | Kingdom | |
"Crash" | Usher | Hard II Love | Mtunzi mwenza, mtayarishaji | |
"Rivals" | ||||
"Helicopters / Beware" | 2017 | Jidenna | The Chief | Mtunzi mwenza |
"Can't Wait" | dvsn | Morning After |