Nenda kwa yaliyomo

Simeoni Mweusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Simeoni Mweusi (au Simeoni Nigeri) alikuwa nabii na kiongozi mmojawapo wa Kanisa la kwanza huko Antiokia, jiji la Siria katika Dola la Roma (leo nchini Uturuki).

Katika kutoa taarifa hiyo, Luka mwinjili (Mdo 13:1) anaeleza kwamba alikuwa mmoja kati ya watano, wakiwemo Barnaba na Paulo.

Kanisa la Antiokia lilianzishwa na Wakristo wenye asili ya Kiyahudi lakini wa lugha ya Kigiriki, waliotawanyika baada ya dhuluma iliyoanza kwa kifodini cha Stefano mjini Yerusalemu (Mdo. 11:19-24).

Inawezekana kwamba Simeoni alikuwa mmojawao.

Anaheshimiwa kama mtakatifu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simeoni Mweusi kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.