Nenda kwa yaliyomo

Copernici

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ununbi)


Copernici (Copernicum, zamani Ununbium)
Jina la Elementi Copernici (Copernicum, zamani Ununbium)
Alama Cn (zamani Uub)
Namba atomia 112
Mfululizo safu matali za mpito (?)
Uzani atomia 277 g/cm³ (kadirio)
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 18, 2
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Asilimia za ganda la dunia 0% (elementi sintetiki)
Hali maada huaminiwa kuwa gesi au kama metali
Mengineyo Copernici / Ununubi ni elementi sintetiki yenye nusumaisha mafupi sana iliyotengenezwa mara nne tu

Copernici (kwa Kilatini: Copernicum, zamani Ununubium) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 112 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 277. Alama yake mpya ni Cn (zamani Uub). Si rahisi kutaja tabia zake kwa sababu imetengenezwa mara nne tu katika maabara kama atomi moja-moja.

Jina lilitolewa kwa heshima ya mwanaastronomia Nikolaus Kopenikus (kwa Kilatini Copernicus). Jina la awali lilitokana na maneno ya Kilatini kwa "1" (unum) na kwa "2" (bi). Un-un-bi yamaanisha hivyo moja-moja-mbili yaani namba atomia ya elementi. Ununbi lilikuwa jina la muda kabla ya wataaalamu hukubaliana.

Ufumbuzi

[hariri | hariri chanzo]

Elementi hiyo iliwahi kutabiriwa na wanasayansi kuwa inaweza kupatikana. Ilitengenezwa mara ya kwanza mwaka 1996 na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt (Ujerumani) kwa kufyatulia viini vya atomi za zinki katika risasi.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Kama elementi zote za sintetiki, hiyo pia haina matumizi bado: zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano wa kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu, kutokana na maisha mafupi ya atomi zake, zimeshapotea muda mrefu.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Copernici kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.