Wikipedia:Istilahi za wiki
Mandhari
CH
[hariri chanzo]- Jamii (Category)
- Jamii ni mkusanyiko wa makala zote zinazohusika na kichwa fulani, pamoja na vijamii vyake; kwa mfano Jamii:Nchi za Afrika. Majina ya jamii zote ambazo ukurasa umewekewa ndani zao yameandikwa mwishoni mwa ukurasa. Kichwa cha jamii zote ni Jamii:Jamii Kuu. Unaweza kutafuta jamii fulani kwa kuingiza Jamii:jina linalotafutwa ndani ya sanduku la kutafuta.
- Maelezo mengine yanapatikana hapa.
- Kijamii (Subcategory)
- Kuna jamii moja tu, Jamii:Jamii Kuu, ambaye si sehemu ya jamii nyingine. Jamii zote zinazoonekana kwenye orodha ya vijamii kwenye ukurasa wa jamii nyingine ni vijamii vyake.
- Mkabidhi (Admin, sysop)
- Mkabidhi ni mtumiaji anayepewa majukumu kadhaa ya kutunza wiki. Anaweza kufuta kurasa, kulinda kurasa na kuzuia watumiaji wanaofanya fujo. Wezo za wakabidhi zinaelezwa katika "Wezo za kundi za watumiaji".
- Mtumiaji (User)
- Mtu anayeandika katika wiki hii au anayefanya kitu chochote katika wiki. Wakati mwyingine mtumiaji anaitwa mhariri. Wezo za watumiaji zinaelezwa katika "Wezo za kundi za watumiaji".