Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA(TaFF)

KUHUSU TaFF

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umeanzishwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Sheria ya Misitu Sura 323 kwa lengo la kuwa chanzo cha uhakika na endelevu cha fedha kwa ajili ya kuwezesha na kugharamia uhifadhi, usimamizi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali misitu hapa nchini. Mfuko huu unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini na shughuli za kila siku zinafanywa na Sekretarieti ya Mfuko.

Kuwa Taasisi inayoongoza kuwa na chanzo cha uhakika na endelevu cha fedha kwa ajili ya kuwezesha na kugharamia uhifadhi, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za misitu.

Kwa niaba ya timu nzima, ninafuraha kukukaribisha kwenye tovuti ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) ambapo unaweza kupata nyenzo na taarifa tunazoamini unazihitaji ili kuelewa kikamilifu, mapana na marefu ya utendaji, dira, dhamira na maadili ya msingi ya TaFF.