


Huduma Zetu
Bodi ina mamlaka ya kisheria ya kusajili Wakulima wa Tumbaku, Wafanyabiashara wa Tumbaku, Vyama vya Msingi vya Ushirika, Vituo vya kuchambulia na kufungia tumbaku na Vituo vya Masoko ya tumbaku. Unaweza kutembelea tovuti hii: e-Kilimo kuomba huduma hizi.
Bodi imepewa jukumu la kutoa leseni na vibali mbalimbali vya kuagiza na kuuza tumbaku nje ya nchi kwa wafanyabiashara wa tumbaku nchini. Baadhi ya leseni hizo ni Leseni ya Kununua Tumbaku Mbichi shambani, Leseni ya kuuza tumbaku iliyosindikwa, Leseni ya usindikaji wa tumbaku na Leseni ya kununua tumbaku iliyosindikwa. Unaweza kuomba huduma hizi kupitia tovuti ya e-Kilimo.
Bodi ya Tumbaku Tanzania ina Maafisa Kilimo waliofunzwa vyema ambao hutoa utalaam, taarifa, uzoefu na teknolojia kwa wakulima wa tumbaku nchini. Ili kuhakikisha ufanisi wa tasnia ya tumbaku nchini, Bodi inatumia mafunzo na ziara za mashambani na mbinu shirikishi za ugani ili kutoa maarifa yaliyokusudiwa kwa wakulima wa tumbaku.
Matukio na Matangazo
Msimu wa masoko ya tumbaku 2025/2026
27 Machi 2025
Mkutano wa tathmini ya zao mwaka 2025
19 Machi 2025
Habari Mpya
Bodi ya Tumbaku yatoa utaratibu wa kuomba leseni za ununuzi wa tumbaku kwa msimu wa masoko 2025/2026
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Bw. Stanley N. Mnozya amewataka viongozi wote ndani ya sekta ya tumbaku kuheshimu taratibu za kilimo cha tumbaku, viongozi wa serikali na kuacha dhuruma dhidi ya wakulima wa zao la tumbaku.
Tazama jinsi Bodi ya Tumbaku Tanzania ilivyompongeza Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuibeba tasnia ndogo ya tumbaku tangu achukue madaraka ya nchi hii