Nenda kwa yaliyomo

Dodoma (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma is located in Tanzania
Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma

The position in Tanzania

Majiranukta: 6°10′S 35°44′E / 6.167°S 35.733°E / -6.167; 35.733
Nchi Tanzania
Mkoa Dodoma
Idadi ya wakazi (2012)
 - Wakazi kwa ujumla 2,083,588

Dodoma ni mji wa Tanzania ya kati. Imetangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973. Hali halisi makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia ikulu halisi ya rais. Lakini bunge hukutana Dodoma na sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma. Mji ni pia makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Dodoma.

Eneo la mji liko 1135 m juu ya UB. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 2,083,588 mwaka 2012. Kiuchumi ni kitovu cha biashara ya kilimo cha karanga, maharagwe na alizeti, pamoja na mifugo na kuku.

Dodoma kuna makao makuu ya Kanisa la Biblia Publishers pamoja na Emmaus Shule ya Biblia.

Mawasiliano

Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Dar Es Salaam au Morogoro - Iringa, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kaskazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya reli ya kati kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma ina uwanja wa ndege wa kitaifa .

Asili ya jina

Neno "Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la kigogo "dodomia" kufuatili historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia.

Historia

Kanisa Kuu la Anglikana, Dodoma Mjini

Dodoma ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo kwenye reli ya kati penye karahana ya reli. Tangu 1912 imekuwa makao makuu ya mkoa. 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja ya mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59.

Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi na maofisi kadhaa ya serikali. Kwa ujumla uhamisho unaendelea kuchelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawapendi kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji mdogo ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Menginevyo kuna matatizo ya kifedha ambayo yamesaidia haidi sasa kutangaza nia ya kuhami lakini kubaki palepale.

Tazama pia

Kata za Wilaya ya Dodoma mjini - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Chahwa | Chamwino | Chang'ombe | Chigongwe | Chihanga | Dodoma Makulu | Hazina | Hombolo Bwawani | Hombolo Makulu | Ihumwa | Ipagala | Ipala | Iyumbu | Kikombo | Kikuyu Kaskazini | Kikuyu Kusini | Kilimani | Kiwanja cha Ndege | Kizota | Madukani | Majengo | Makole | Makutupora | Matumbulu | Mbabala | Mbalawala | Miyuji | Mkonze | Mnadani | Mpunguzi | Msalato | Mtumba | Nala | Nghong'onha | Nkuhungu | Ntyuka | Nzuguni | Tambukareli | Uhuru | Viwandani | Zuzu