San Salvador
Mandhari
San Salvador ni mji mkuu wa El Salvador katika Amerika ya Kati pia mji mkubwa wa nchi hii mwenye wakazi 485,847 (2001) ambao ni theluthi moja wa watu wote nchini.
Jina la mji lamaanisha "Mtakatifu Mwokozi" kwa Kihispania likimaanisha Yesu Kristo.
San Salvador iko kwenye kimo cha m 668 juu ya UB. Imeathiriwa mara kwa mara na mitetemeko ya ardhi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mji ulianzishwa mwaka 1528 na conquistador Mhispania Gonzalo de Alvarado. 1824 baada ya uasi wa koloni za Hispania katika Amerika ya Kati ulikuwa mji mkuu wa shirikisho la Amerika ya Kati. Baada ya kuachana kwa umoja hu ulikuwa mji mkuu wa El Salvador tangu 1841. Categorie:Miji Mikuu Amerika