Nenda kwa yaliyomo

Zambia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Republic of Zambia
Jamhuri ya Zambia
Bendera ya Zambia
Bendera ya Zambia
Neno Kuu: “One Zambia, one nation”
Kiing. „Zambia moja, Taifa moja“
Lugha rasmi Kiingereza
Mji Mkuu Lusaka
Serikali Jamhuri
Rais Hakainde Hichilema
Eneo 752.614 km²
Idadi ya Wakazi 17,351,708 (Julai 2018)
Wakazi kwa km² 17,2
Uhuru Kutoka Uingereza 24 Oktoba 1964
Pesa Kwacha ya Zambia = 100 Ngwee
Wakati UTC+2
Wimbo wa Taifa Lumbanyeni Zambia (Stand and sing of Zambia)
Ramani ya Afrika inayoonyesha Zambia
Ramani ya Afrika inayoonyesha Zambia
Ramani ya Zambia

Jamhuri ya Zambia ni nchi ya Kusini mwa Afrika isiyo na mwambao baharini.

Imepakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania upande wa kaskazini, Malawi upande wa mashariki, Msumbiji, Zimbabwe na Botswana upande wa kusini, Namibia na Angola upande wa magharibi.

Mji mkuu ni Lusaka (wenye wakazi 1,747,152 mwaka 2010).

Jina limetokana na mto Zambezi. Jina la zamani za ukoloni (hadi 1964) lilikuwa "Northern Rhodesia".

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Nchi kwa sehemu kubwa ni nyanda za juu kuanzia mita 1.000 hadi 1.400 juu ya UB. Milima ya Muchinga imepanda hadi mita 2.164, kilele cha juu kabisa kiko kwenye mita 2.301 huko milima ya Mafinga Hills.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na Watwa.

Katika karne za kwanza za milenia ya 1 BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Baada ya wapelelezi Wazungu kufika katika karne ya 18, Zambia ikawa nchi lindwa ya Uingereza kwa jina la Northern Rhodesia mwishoni mwa karne ya 19.

Tarehe 24 Oktoba 1964, Zambia ikawa huru na waziri mkuu Kenneth Kaunda akawa rais wa kwanza.

Chama chake cha kijamaa United National Independence Party (UNIP) kilitawala kuanzia mwaka 1964 hadi 1991, kikiwa chama pekee halali kuanzia mwaka 1972.

Baada ya Kaunda kuanguka, Frederick Chiluba wa Movement for Multi-Party Democracy alitawala tangu mwaka 1991, akafuatwa na Levy Mwanawasa (2002-2008).

Aliyefuata tena ni rais Rupiah Banda (2008-2011), halafu Michael Sata wa Patriotic Front party (2008-2014).

Baada ya kifo chake, Guy Scott alikaimu hadi uchaguzi wa tarehe 20 Januari 2015, ambapo Edgar Lungu alipata kuwa rais wa sita.

Wakazi wa Zambia ni wasemaji wa lugha za Kibantu katika makabila 73. Makubwa ndio Wabemba (19%), Watonga (13.6%), Watumbuka, Wachewa, Walozi, Walunda, Waluvale, Wakaonde, Wankoya na Wanyanja-. Hata hivyo lugha rasmi ni Kiingereza.

Idadi kubwa ni wakulima wa kujitegemea, ingawa 44% wanaishi mijini.

Upande wa dini, karibu wote ni wafuasi wa Ukristo ambao ndio dini rasmi kwa mujibu wa katiba ya nchi. 75.3% ni Waprotestanti, 22% ni Wakatoliki na wengine wana dini ya aina nyingine au ni wakanamungu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zambia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.