Majambazi Quotes

Quotes tagged as "majambazi" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Majambazi huwapenda wanaowapenda. Chukulia mfano huu: Mimi na Wanda ni marafiki, OK? Baba yake, au genge la baba yake, hataweza kunidhuru au kuwadhuru watu ninaowapenda kwa sababu tu ya urafiki na mtoto wake. Na yeye anaweza kufumbiwa macho akifanya makosa kwa sababu mimi na mtoto wake ni marafiki wakubwa. Murphy, hapa Meksiko tuna kitu kinaitwa Bima ya Utekaji Nyara ('Ransom Insurance'). Zamani nilikuwa nalipa dola milioni kumi za Marekani kama bima ya utekaji nyara; Lisa alikuwa analipa milioni nne na Wanda bado analipa milioni mbili mpaka sasa hivi. Baada ya mimi na Lisa kujenga urafiki na Wanda, malipo yetu ya bima yamepungua mpaka dola milioni moja kwa mwaka.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Debbie alilia. Alilia kwa nguvu zake zote. Alijua tayari alishampoteza Murphy na yote yale huenda alisababisha yeye. Bila kujuana na Vijana wa Tume huenda wasingepigwa. Debbie Hakukata tamaa. Alikumbuka kitu halafu akamwita dereva. Alimwomba dereva amkimbize Roma Notre haraka ilivyowezekana. Alidhani alijua majambazi walikokuwa wakikimbilia na kuna kitu alitaka kufanya. Dereva akamkubalia na kuondoka kuelekea Roma Notre. Njiani Debbie hakuacha kulia. Aliwaza alivyompoteza Marciano, akawaza kumpoteza na Murphy. Jibu alilolipata ni kumwokoa Murphy kwa gharama yoyote ile.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita