Maajabu Quotes

Quotes tagged as "maajabu" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Dunia huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka jua. Jua huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka falaki. Dunia hutumia takriban siku moja kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban mwaka mmoja kuzunguka jua. Jua hutumia takriban siku ishirini na tano kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban miaka milioni mia mbili na hamsini kuzunguka falaki. Yoshua alisimamisha jua ili lisizunguke kwenye mhimili wake na lisizunguke falaki. Kwa sababu jua lilisimama, kila kitu kilichoathiriwa na jua hilo kilisimama pia ikiwemo dunia. Hata hivyo, kwa sababu tukio la Yoshua kusimamisha jua na mwezi yalikuwa maajabu kutoka kwa malaika wema, malaika wema ndiyo wanaojua kwa hakika nini kilitokea. Yoshua alikuwa sahihi kusema jua lisimame si dunia isimame. Mungu aliweza kusimamisha jua kwa ajili ya Yoshua kuwashinda maadui zake, kwa sababu aliamini. Mungu anaweza kusimamisha jua kwa ajili yako kuwashinda maadui zako, ukiamini. Mungu anapokuwa na wewe matatizo yako yako matatizoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wanaamini kuwa Yesu atarudi tarehe 29 Julai 2016. Tarehe hiyo kitu kikubwa sana kitatokea katika dunia yetu kitakachosababisha tetemeko kubwa la ardhi, litakalosababishwa na kubadilika kwa ncha za dunia, tendo litakalosababisha mionzi ya gama kutoka kwenye jua ifike duniani na kuua kila kitu kinachoonekana katika uso wa dunia hii. Watakatifu watafufuka na kumlaki Kristo mawinguni, ambaye anakuja kuwachukua wateule na kumweka Shetani kifungoni kwa miaka 1000. Hayo yote, wanasema, yatatokea ndani ya siku 11 kuanzia leo. Yaani, kusini mwa dunia kutakuwa kaskazini mwa dunia, kaskazini mwa dunia kutakuwa kusini mwa dunia.

Kitendo hicho kitafanya dunia ikose kinga ya sumaku iitwayo ‘magnetosphere’ ambayo hukinga dunia dhidi ya mionzi ya gama kutoka kwenye jua. Mionzi hiyo hugonga ukuta wa ‘magnetosphere’ kila baada ya dakika 8 kwa mwendokasi wa kilometa milioni 1080 kwa saa; na kusambazwa katika ncha za dunia ambapo aghalabu huchanganyikana na oksijeni na kutengeneza kitu kinaitwa ‘aurora’, au mwanga wa ncha, ambacho ni maajabu mengine ya angani. Mwaka 2012 wanasayansi walisema ncha za dunia zingebadilika lakini hazikubadilika. Je, muda umefika sasa wa kuwaamini wanasayansi? Biblia ni chuo cha Mungu. Soma Biblia kupata maarifa.”
Enock Maregesi