Nadhiri Quotes

Quotes tagged as "nadhiri" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta – kwa sababu hata mimi nilikuwepo – na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitamka nadhiri waziwazi Shetani atasikia. Akisikia atavuruga. Mipango yako yote aliyosikia itakuwa matatizoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani anatesa mwili si roho. Nadhiri ni siri ya rohoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nadhiri ni siri.”
Enock Maregesi