Shetani Quotes

Quotes tagged as "shetani" Showing 1-30 of 92
Enock Maregesi
“Lengo kuu la Shetani kuingilia uumbaji wa Mungu kwa kutumia Succubus na Incubus ni kumzuia Yesu asirudi kwa mara ya pili. Anajua akiingilia uumbaji huo na kuwafanya watu wote wawe na roho za kishetani, wokovu hautakuwa na maana, Yesu hatakuwa na mtu wa kumwokoa atakaporudi kwa mara ya pili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Jina la Yesu ni kubwa kuliko majina yote duniani na hata kuzimu. Lazima Shetani aliogope kuliko anavyomwogopa Bikira Maria au sakramenti za aina zote. Kumbuka, jina la Yesu halitajwi kilingeni. Linatajwa kanisani, ambapo linatajwa kinafiki. Hivyo, aliye na mamlaka ya kuaminiwa na kuabudiwa na aponyaye ni Yesu Kristo peke yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama Mungu na Shetani hawako ndani yako, hiyo vita ya kiroho unaipigania wapi?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kutoka nyumbani kwako hadi kazini kwako na kutoka kazini kwako hadi nyumbani kwako, umeepuka wastani wa mitego 10,000 ya Shetani! Kuwa na huruma kwa malaika anayekulinda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ndugu zangu, malaika wanatulinda. Wako katikati ya maadui zetu na sisi. Hatujui ni mara ngapi malaika wameingilia kati kuokoa maisha yetu, kutuepusha na nguvu za Shetani na malaika wake wakorofi. Lakini nina hakika ya kwamba wamefanya hivyo mara nyingi katika mazingira ambapo aghalabu sisi huwa hatuelewi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Toa msamaha usiokuwa na masharti yoyote kwa yeyote aliyekukosea kwa sababu, dhambi iliyofanya mkosane ilitoka kwa Shetani. Kwa mfano, usiseme umesamehe lakini hutasahau, sema umesamehe na umesahau.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ongea na Mungu kimoyomoyo ili Shetani asisikie.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hawezi kuona wala kusikia kinachoendelea ndani ya moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu alikuwa binadamu ili afe kama binadamu kwa ajili ya binadamu. Alikufa msalabani ili sisi wote tuokoke. Lakini Shetani hataki hilo litokee. Akiingilia uumbaji wa Mungu toka tumboni mwa binadamu, binadamu atakayezaliwa hatakuwa na uwezo wa kuongoka. Atakuwa na roho ya jini itakayomjua Shetani badala ya kumjua Mungu. Hivyo kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili hakutakuwa na maana, kwa sababu hakutakuwepo na mtu wa kuokolewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata hivyo, toka mwaka 1995 watu wengi walianza kuamka kiroho dunia nzima; na mwaka 2012 waliamka zaidi, pale ulimwengu ulipoanza kuhama kutoka kwenye masafa ya ngazi ya nne ya ufahamu wa binadamu (‘4th dimension’) kwenda kwenye masafa ya ngazi ya tano ya ufahamu wa binadamu (‘5th dimension’) inayohusika zaidi na ulimwengu wa roho na ambayo bado inaendelea kuhama mpaka dakika hii. Ndiyo maana watu wengi zaidi wanamjua Mungu kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote kile katika historia ya dunia yetu. Kwa sababu hiyo, Shetani hatashinda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hawezi kujua unafikiria nini: 1 Wafalme 8:39. Yesu anajua unafikiria nini: Yohana 2:25. Shetani haweza kufanya jambo bila ruhusa ya Mungu: Mathayo 4:1. Shetani hawezi kukulazimisha kutenda dhambi: Yakobo 4:7. Pigana na mwindaji wa roho hadi roho yako ikombolewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kufanikiwa lazima umshinde Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani usimchokoze. Ukimchokoza anakuvaa kwelikweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitamka nadhiri waziwazi Shetani atasikia. Akisikia atavuruga. Mipango yako yote aliyosikia itakuwa matatizoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani anatesa mwili si roho. Nadhiri ni siri ya rohoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Bila kiburi hutamshinda Shetani, lakini kiburi dhidi ya Shetani unakishinda kwa hekima.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kumbuka, ukimrudishia Shetani tusi utakuwa umejitukana mwenyewe; kwa sababu kile unachokiona nje kiko ndani yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hatawasamehe wanadamu kwa sababu ya kiburi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani anapunguza umaskini kwa kuua maskini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wenye dhambi watafufuliwa na wataungana na Ibilisi kuipiga Yerusalemu Mpya itakayokuwa inang'inia hewani, huku Yesu na watakatifu wote wakiwa hawana silaha yoyote; lakini vilevile wakiwa hawapigwi kwa silaha yoyote.

Shetani atakapoonekana kushindwa, Yesu atawasha ‘kibiriti cha kiroho’. Mafuta yote yaliyopo ardhini dunia nzima yatalipuka na kugeuza ardhi yote kuwa ziwa la moto, na hivyo wenye dhambi wote kupata aibu ya milele.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Roho ikikua itajua hiki ni cha Mungu na hiki ni cha Shetani! Chaguo ni lako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukikasirika, aliyesababisha ukasirike ni Shetani aliyeko ndani yako; na ukiwa na furaha, aliyesababisha uwe na furaha ni Mungu aliyeko ndani yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Taifa ni malaika! Taifa ni Shetani! Laana ya mwenye haki ina haki.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani ni profesa wa saikolojia! Lakini, ukiwa msiri, hatakupata.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Manabii wa uongo, na wafuasi wao, hawautaki ukweli. Kazi yao ni kutulazimisha tumwabudu Mpinga Kristo, badala ya Yesu Kristo, bila sisi wenyewe kujua. Wana mamlaka yote ya Mpinga Kristo kwa sababu, kama Mpinga Kristo, wanaongozwa na Shetani. Walimu hawa wa uongo wanaopenda kuvalia misurupwenye ya kisawasawa, na wanaoongea utafikiri wamemeza Biblia na kuitapika kwenye mikrofoni, lengo lao ni kutupeleka kwenye ufalme wa Shetani. Hatuna budi kuitangaza injili ya kweli ya Yesu Kristo, kwa imani ya kweli, kupata urithi usiohongeka wa ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Manabii wa uongo wana dhambi kuu tatu: tamaa ya ngono, uasi dhidi ya mamlaka ya Kristo, na dharau kwa Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nabii wa uongo atampinga Shetani kwa nguvu zake zote, atakuwa na tamaa ya wanawake au wanaume kama ilivyokuwa kwa Sodoma na Gomora na miji yote iliyoizunguka miji hiyo, na atayadharau mamlaka ya Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu angekuwa anababaishwa na mwili asingeruhusu Shetani autese mwili wa Ayubu kiasi chote kile isipokuwa roho yake, wala tusingekuwa tunateseka, wala watoto wadogo wasingekuwa wanakufa, wala watu wasiokuwa na hatia wasingekuwa wanakufa vitani au katika majanga mengine yoyote yale katika dunia hii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote mbele ya Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hawezi kusoma ndani ya myoyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Usimpe nafasi Shetani.”
Enock Maregesi

« previous 1 3 4