Tajiri Quotes

Quotes tagged as "tajiri" Showing 1-30 of 31
Enock Maregesi
“Kama una akili kuwa kawaida. Kama una nguvu kuwa mkarimu. Kama una pesa kuwa mnyenyekevu. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa na pesa kuwa mnyenyekevu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini na tajiri wana mawazo tofauti. Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo. Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo. Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri. Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake. Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana. Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani. Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa. Maskini ana woga. Tajiri hana woga. Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi. Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake. Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo. Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini ana woga. Tajiri hana woga.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa na mafanikio ya Shetani hayo si mafanikio ya kweli. Ukiwa na mafanikio ya Mungu hayo ndiyo mafanikio ya kweli. Mafanikio ya kweli hayatokani na NINI unacho. Mafanikio ya kweli yanatokana na NANI unaye. Yesu Kristo alikuwa maskini, hakuwa na kitu; lakini alikuwa tajiri, alikuwa na Mungu ndani ya moyo wake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ina thamani pale unapokuwa nayo, si pale unapokuwa huna, hivyo iweke mahali unapoweza kuiona: katika nyumba, katika shamba au katika elimu. Badala ya kumpa mtu pesa ili ajenge nyumba, mpe nyumba. Badala ya kumpa mtu pesa ili afanye biashara, mpe biashara. Halafu, mpe elimu afanye maamuzi ya biashara yake. Pesa ina laana na Mungu pekee ndiye anayeweza kuiondoa laana hiyo. Ni rahisi kwa tajiri kupata baraka ya pesa kwa sababu ana pesa na ana uwezo mkubwa wa kusaidia maskini. Ni vigumu kwa maskini kupata baraka ya pesa kwa sababu hana au ana uwezo mdogo wa kusaidia maskini. Mungu anaweza kuondoa laana ya pesa kupitia hisani kwa maskini, kitu ambacho aghalabu hufanywa na matajiri wenye uwezo mkubwa. Heri kutoa kitu au huduma au elimu kwa maskini kuliko pesa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utajiri wa mbinguni ni wa milele na mungu wake ni Yehova. Utajiri wa duniani ni wa muda na mungu wake ni Mammon. Mammon, ambaye hata Yesu alimtaja katika Injili ya Mathayo 6 na katika Injili ya Luka 16, ni mungu wa uchoyo na utajiri wa dunia hii. Mammon kazi yake ni kufanya watu waliokufa kifedha na walio hai kifedha kuwa maskini wa milele ahera. Yesu Kristo alikuwa maskini, ili tuwe matajiri kupitia umaskini wake, lakini kwa sababu alikuwa na imani ya Mungu katika moyo wake alikuwa tajiri. Hivyo unaweza kuwa na utajiri wa mbinguni hapa duniani, ukiikaribisha amani ya Mungu katika moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwaza kwa kufuata kanuni ya nguvu ya uvutano (ambayo ni kuwaza na kuamini kama kile unachokiwaza tayari umeshakipata bila hata kujua umekipataje) utaishi kama ulivyowaza. Ukiwaza kuwa jambazi utakuwa jambazi hakika, ukiwaza kupona ugonjwa unaokusumbua utapona hakika, na ukiwaza kuwa tajiri utakuwa tajiri hakika. Mafanikio hayo yanaweza kuchukua mwezi mmoja kutimia au yanaweza kuchukua miaka kumi. Unachotakiwa kufanya ni kuwaza na kuamini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utajiri una changamoto nyingi. Yesu alisema ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Hakusema msomi. Usiwe mwendanguu. Jikusuru kuujua ukweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba utajiri una changamoto nyingi kuupata na kuudumisha pia kuliko usomi na kwamba ukweli ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. Heri msomi kuliko tajiri – Heri yule aliyesoma kuliko tajiri asiyesoma au yule aliyesoma kuliko vile alivyosoma tajiri au tajiri asiyesoma au aliyesoma lakini asiyekuwa na tamaa kabisa na dunia hii ambaye kukosa kwake tamaa na dunia hii kunamfanya msomi. Ndivyo Kristo anavyomaanisha. Si kwamba tajiri hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu, Daudi, Sulemani, Yehoshafati, Hezekia, Zakayo, Yoana, Susana, na Lidia watauona ufalme wa mbinguni na walikuwa matajiri. Mali zao zilivyozidi hawakuangalia moyoni, hawakuwa na tamaa kabisa na dunia hii, bali walimtumaini Mungu kwa kila kitu walichokuwa nacho. Anaweza. Lakini asiipende dunia bali ayapende mambo ya ufalme wa Mungu kwa moyo wake wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tajiri asiyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia au yule aliyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia ni msomi. Anaweza kuuona ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Bila maskini tajiri hana maana!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tajiri bila maskini ni maskini na bila tajiri maskini ni tajiri. Tajiri akiwa na maadili, maskini atakuwa tajiri.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Huwezi kuwa tajiri iwapo wewe ni limbukeni wa hela.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Bila tajiri huwezi kuwa tajiri wa kupindukia.”
Enock Maregesi

« previous 1